Vingozi wa Jumuiya za Usharika wa Kijitonyama wanatarajiwa kuingizwa kazini katika Ibada ya Jumapili tarehe 20 Februari 2022.
Viongozi hao wanatarajiwa kuingizwa kazini kutumikia Jumuiya zao kwa kipindi cha miaka miwili. Hivi karibuni Dayosisi ilitoa mwongozo kwa Jumuiya zote kufanya uchaguzi wa viongozi wake.
Usharika wa Kijitonyama una jumla ya Jumuiya 14 ambazo ni Msifuni, Nuru, Agape, Sifuni, Mikocheni/Regency, Tumaini na Sayuni.
Jumuiya nyingine za Usharika ni Upendo, Ebenezer, Angaza, Hosiana, Amani, Neema na Amkeni.