Morning And Evening Glory
Shule ya Uponyaji ni mafundisho yenye msingi wa Kibiblia yenye lengo la kuwezesha watu wa rika na madhehebu yote kuponywa Kiroho, Kimwili, Kiakili na Kifikra kwa njia ya kumjua Mungu na kufahamu kusudi la Mungu kwa mwanadamu na kuishi maisha yanyoendana na kusudi la Mungu na viwango amavyo Mungu amevikusudia kwake.
Msingi wa Shule ya Uponyaji ni kutoka Methali 1: 1-7; ambao uanlenga kujua matendo makuu ya bwan ili kujua hekima na adabu, kutambua maneno ya ufahamu, kufundishwa matendo ya busara katika haki, hukumu na adili, kuwapa wajinga werevu. Kuwapa vijana maarifa na hadhari, kuwaongezea elimu wenye hekima, na wenye ufahamu mashauri yenye hekima.
Shule hii ya Uponyaji inatambua umuhimu wa katika maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla na kuwa vijana wengi wanahitaji kupewa maarifa na hadhari ili kuwajenga katika msingi ambayo itawasaidia kujituma katika kufanya maendeleo ambayo yataleta mabadiliko makubwa kwa Tanzania na Ulimwengu. Mafundisho haya yatawasaidia vijana kupata maarifa ya kuona fusara zenye Baraka za Kimbingu na hadhari katika maisha yao.
Shule ya Uponyaji inaambatana na Ushauri wa Kichungaji unaofanyika kila mwezi Septemba lengo likiwa ni kutoa ushauri nasaha ili kuwafungua watu na kuponya jeraha zao, Majadiliano ili kutoa fursa ya kupokea shuhuda mbalimbali na kuona jinsi ambavyo watu wamefanikiwa ili kuwatia moyo wengine na kupata mbinu, ujuzi na maarifa ya kufanikiwa kupitia misingi ya Kibiblia.
Shule ya Uponyaji inawaleta watumishi wa kitheologia toka madhehebu mbalimbali, wachumi, wafanyabishara na wataalamu wa fani mbalimbali ili kuhudumia kanisa la Mungu. Shule hii inaongozwa na Mch. Eliona Kimaro ambaye ni Mchungaji Kiongozi Usharika wa Kijitonyama.
Jumatatu hadi Ijumaa
Evening Glory: Saa 12:00 - 2:00 Jioni