Usharika uliagana rasmi na Baraza la Wazee lililotumika kwa miaka minne (2018-22) katika Ibada iliyofanyika tarehe 09 Julai 2023.
Baraza hilo lililotumika Usharikani chini ya uongozi wa Katibu wa Baraza Dkt. Victoria Kisyombe, lilijumisha Wazee 33 ambao walichaguliwa kuwa Wazee wa Kanisa mwaka 2018.
Bwana Mungu awabariki Wazee wote wastaafu kwa huduma njema ya utumishi nyumbani mwa Bwana.
