Mpendwa Msharika,
Bwana Yesu Kristo asifiwe!!
Tunapenda kukukaribisha kwenye Ibada ya Kusifu na Kuabudu itakayoambatana na Utoaji wa Zaka Kamili (Fungu la Kumi) siku ya Jumapili tarehe 05 June, 2022.
Ibada itakuwa MOJA na itaanza saa 1:00 asubuhi.
Ibada itaambatana na Maombi Maalum kwa watu wote wenye mahitaji mbalimbali
Watoto wote wataingia kwa maandamano na kuombewa kwenye Ibada ya watu wazima na baadaye watasali katika madarasa yao
Tena kwao itasikiwa shukrani, na sauti yao wachangamkao; nami nitawazidisha, wala hawatakuwa wachache; tena nitawatukuza, wala hawatakuwa wanyonge. Yeremia 30:19
Mungu akubariki!
