Umoja wa Wakinamama

Kwaya Ya Uamsho Kijitonyama

Historia

Kwaya ilianzishwa mnamo 20/04/1996, ilikwa kwaya ya fellowship ikiwa na waimbaji sita (6) kwa sasa kwaya ina jumla ya wanakwaya thelathini na tano (35). Kwaya Uamsho ni mwanachama wa Umoja wa Kwaya za Uinjilisti na Uamsho jimbo la Kinondoni (UKUU) na Umoja wa Kwaya za Uinjilisti na Uamsho wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani (UKUD).

Dira Yetu

Dira ya Umoja wa kina mama ni kuwa kikundi bora chenye kumjua MUNGU nakuwa na miradi yenye tija ya kuweza kusaidia wanawake na mabinti wenye uhitaji.

Dhima Yetu

Dhima ya kikundi hiki ni kuwa na umoja na mshikamano mkubwa kuweza kuwa mfano mzuri kwa wanaotuzunguka na kuwa na upendo popote tunapokuwa.

Malengo Yetu

Kuwa wamama waombaji pia wamama,kuwa na iradi ya kudumu mfano ushonaji, upishi, upambaji, kuwa na firm ya usafi na utunzaji bustani ili tuweze kuajiri wale ambao wana shida mbalimbali waweze kufurahia kipato kutoka kwenye umoja wa wamama,pia kuwa na stationary yetu kwani tuna watu wenye uzoefu wa Nyanja zote hizo.

Sifa Za Kujiunga na Umoja wa Wakinamama

  1. Awe mama msharika
  2. Mcha Mungu
  3. Awe anashiriki meza ya Bwana
  4. Awe kwenye jumuiya zetu
  5. Awe amejiandikisha na ana namba ya ahadi n.k.

Kazi Mbalimbali Za Umoja Wa Wakinamama

  1. Kutembelea wagonjwa
  2. Kutembelea waliofiwa
  3. Kufanya usafi usharikani
  4. Kukutana na mabinti wenye kuhitaji huduma kutoka kwa wanawake wazee
  5. Kupokea wageni toka nje na ndani ya Dayosisi n.k.

Uongozi na Mawasiliano

Cheo Jina Mawasiliano
Parish worker Neema Kisyala 0655 774831
Mwenyekiti Emma Mushi 0715 352579
M/Mwenyekiti Bertha Kijo 0762561052
Katibu Mkuu Neema Kisasa 0755096184
Katibu Msaidizi Sophia Mwita 0655364743
Mweka hazina Nora Kahwa 0713 373715
M/Mweka hazina Mary Mhando 0682 565931