Darasa La Kipaimara

Ibada

Huduma Ya Darasa La Kipaimara

Hii ni huduma inayotolewa ili kuwaimarisha na kuwajenga watoto katika Imani ya kikristo ili kuimarisha maisha yao ya kiroho na kimwili, pia kuongeza ufahamu wao juu ya uwezo na ukuu wa Mungu katika maisha yao. Hii huwasaidia kuwandaa kuwa wakristo imara katika kumtumikia Mungu na kuutangaza ukuu wake na kumshuhudia Kristo.

Mafundisho ya Kipaimara yanatolewa kwa miaka miwili kwa watoto wenye umri kati ya miaka 11-12. Hufanyika mara mbili kwa wiki katika siku za Alhamisi na Jumamosi. Siku ya Alhamisi yanaanza saa 11-12 jioni na siku ya Jumamosi yanaanza saa 3-5 asubuhi. Mafundisho huratibiwa na Ofisi ya Mwinjilisti, ambapo huhusika pamoja na mambo mengine katika kuandikisha watoto, kuwafundisha na kuwajaribu kabla ya kupata kipaimara.

Darasa La Nikodemu

Darasa hili ni mahususi kwa mafundisho ya kipaimara na ubatizo kwa watoto wenye umri wa miaka 15 au zaidi na kwa watu wazima. Utaratibu wa kujiunga na Darasa hili hutolewa katika matangazo ya usharika na pia katika ofisi ya Mwinjilisti wa Uaharika. Mwanafunzi hubarikiwa au kubatizwa baada ya kupimwa hivyo darasa hili halina muda maalumu wa kuhitimu hutegemea Zaidi uelewa wa wanafunzi. Mafundisho hayo hutolewa siku za Jumatano na Ijumaa saa 10-11 jioni.

Muda

Alhamisi
saa 11-12 jioni
Jumamosi
saa 3-5 asubuhi