Ibada
Huduma Ya Ibada Za Jumapili
Kuna ibada mbili ambazo hutolewa kwa lugha ya Kiswahili, ibada ya kwanza huanza saa moja kamili na ya pili huanza saa nne kamili asubuhi. Ibada hizi huambatana na huduma mbalimbali kama vile
- Ubatizo wa watoto na watu waziama, ubatizo ni mara moja kwa mwezi isipokuwa pale inapotokea dharura, hufanyika siku ya Jumamosi.
- Sakramenti ya meza ya Bwana ambayo hufanyika mara moja kwa mwezi na pia huduma hii hutolewa kwa wagonjwa hospitalini au nyumbani.
- Fungu la Kumi ambalo hutolewa kila jimapili ya kwanza ya mwezi.
- Ibada ya kusifu na kuabudu ambayo hufanyaika kila jumapili ya mwisho wa mwezi.
- Ibada ya mkesha wa maombi ambayo ambayo hufanyika kila ijumaa ya mwisho wa mwezi.
- Shukrani hii hufanyika kila siku wakati wa ibada,ambapo washarika humshukuru Mungu kwa matendo makuu aliyowatendea.
- Ibada ya ndoa hufanyika kila siku ya Jumamosi kuanzia saa tisa alasiri ispokuwa kipindi cha Kwaresma ambapo ibada hii haitolewi isipokuwa kwa kibali maalum. Usharika pia hutoa huduma ya ndoa za pamoja kwa washarika waliokaa muda mrefu bila kubariki ndoa au wenye ndoa za serikali. Ndao hizi hufungwa pale panapokuwa kunauhitaji.
Muda wa Ibada
Ibada ya kwanza
saa moja hadi saa nne kamili
(1:00 – 4:00) asubuhi.
Ibada ya pili
saa tano asubuhi hadi saa saba mchana
(5:00- 7:00)
saa moja hadi saa nne kamili
(1:00 – 4:00) asubuhi.
Ibada ya pili
saa tano asubuhi hadi saa saba mchana
(5:00- 7:00)