Kusifu na Kuabudu

Kikundi cha Kusifu na Kuabudu

Utangulizi

Kikundi cha Kusifu na Kuabudu (Praise and Worship Team) ni moja ya vikundi vya Usharika wa Kijitonyama kilichoanzishwa na Ofisi ya Mchungaji Kiongozi.
Kusifu na Kuabudu

Malengo Ya Kikundi

  1. Kuongoza Kusanyiko kwenye kumsifu na kumwabudu Mungu.
  2. Kuibua vipawa vya Washarika waimbaji hasa katika eneo la kusifu na kuabudu (Worshipers).
  3. Kuwafundisha wale walioibuliwa jinsi ya kuongoza sifa na kuabudu.
Lengo Kuu La Kikundi
Kuongoza kusanyiko (congregation) katika kumsifu na kumwabudu Mungu wakati wa Ibada mbalimbali za Usharika.

Sifa za Kujiunga na Kikundi

  1. Awe Mkristo na mwenye kipawa cha kuimba
  2. Mkristo aliyekatashauri na kumpa Yesu maisha
  3. Mkristo mwenye ushuhuda wa maisha safi.

Walengwa

Kila Mkristo mwenye kipawa cha kuimba hasa nyimbo za kusifu na kuabudu (Worshipers)

Nyimbo / Matoleo Mbalimbali

Toleo Jina
Toleo la kwanza nyimbo za kwaresima
Toleo la pili nyimbo za Pasaka(kufufuka)
Toleo la tatu nyimbo za kupaa na kushuka kwa Roho Mtakatifu

Ratiba Ya Mazoezi

Ratiba ya mazoezi ya maandalizi ya Ibada ni kila siku baada ya Ibada za Morning na Evening Glory.

Viongozi Wa Kwaya

Kikundi kinalelewa na Kamati ya Uingilisti na Misioni na kinaongozwa na

Cheo Jina
Mratibu Amani Kimwaga
Mwalimu James Mbilizi

Mawasiliano

  1. Ofisi ya Mchungaji Kiongozi
  2. Usharika wa Kijitonyama