Kwaya Ya Uamsho Kijitonyama
Historia
Kwaya ilianzishwa mnamo 20/04/1996, ilikwa kwaya ya fellowship ikiwa na waimbaji sita (6) kwa sasa kwaya ina jumla ya wanakwaya thelathini na tano (35). Kwaya Uamsho ni mwanachama wa Umoja wa Kwaya za Uinjilisti na Uamsho jimbo la Kinondoni (UKUU) na Umoja wa Kwaya za Uinjilisti na Uamsho wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani (UKUD).
Dira
Kuwafikia watu wote wasiomjua Mungu maeneo ya misioni.
Dhima Ya Kwaya
Kuhubiri Injili ya Yesu Kristo kwa njia ya uimbaji kwa watu wote ili sawasawa na agizo la Yesu katika Mathayo 28:16-20
Sifa Za Kujiunga na Kwaya
- Awe umeokoka na kumkiri Yesu kuwa ni Bwana na Mwokozi wa maisha yake
- Awe anshiriki Jumuiya na ibada zote.
- Awe na namba ya ahadi ya Usharika.
Lengo Kuu La Kwaya
Kuhubiri injili ya Yesu Kristo kwa njia ya Uimbaji ili kuwa vuta watu kwa Mungu ili wa okoke na kumjua Mungu.
Malengo
Kuhubiri injili kwa njia ya nyimbo, kuwasaidia wahitaji maalumu,kujifunza neno la Mungu(bible study) na maombi.
Walengwa
Wakristo na wasio wakristo.
Nyimbo / Matoleo Mbalimbali
Cheo | Jina |
Mwenyekiti | SAMSON BEGASHE |
M/Mwenyekiti | DOMINICK GABRIEL |
Katibu | JOYSTER NKYA |
Naibu Katibu | NAOMY ABEL |
Ratiba Ya Mazoezi
Mazoezi hufanya mazoezi siku za Jumanne, Alhamisi na Jumamosi kuanzia saa 12 jioni hadi saa 2 usiku.