Shule Ya Jumapili

Ibada

Huduma Ya Shule Ya Jumapili

Usharika unahuduma ya ibada ya watoto, ambayo hutolewa kwa lugha ya Kiswahili na kiingereza. Watoto hugawanywa katika makundi kulingana na umri ili kujenga uelewa kwa watoto. Ibada ya watoto inaambatana na mafundisho ya neno la Mungu, Ibada hii inafanyika kila jumapili katika ibada ya kwanza na ya pili. Watoto hujifunza neno la Mungu pamoja kushiriki katika vikundi mbalmbali kama vile maigizo, kwaya, ngonjera, mashairi, jiving n.k ili kuwakuza kiroho na kimwili. Huduma hii inasimamiwa na ofisi ya Parish worker na inahudumiwa na waalimu wa kujitolea wapatao 19.

Idadi ya watoto hubadlika mara kwa mara ila kwa sasa ni kati watoto 450. Watoto wa shule ya jumapili wanashiriki katika matukio mbalimbali ya Jimbo na Dayosisi.

Muda wa Ibada

Ibada ya kwanza
saa moja hadi saa nne kamili
(1:00 – 4:00) asubuhi.

Ibada ya pili
saa tano asubuhi hadi saa saba mchana
(5:00- 7:00)