Tarumbeta
Dira Ya Kikundi
- Kuwa na wapigaji 150 wa Tarumbeta ambao watafanya muziki wa tarumbeta usikike kwa uzuri zaidi.
- kuanzisha darasa la Tarumbeta kwa watoto na watu wazima hasa wa Usharika huu mfano kwa wanafunzi wa darasa la Kipaimara na Sunday School kuwa na darasa asubuhi na darasa la watu wazima litakuwa jioni ili kuwa na kundi ambalo linaweza kugawanyika mara mbili katika Ibada ya kwanza na pili.
- Kila Mwaka tuwe na wahitimu wanaojua kusoma muziki kwa ufanisi; kuupiga muziki kwa ustadi kwa kufanya hivyo kutawafanya vijana wetu waenende na kasi ya Dunia iliyopo hasa utandawazi kwenye tasinia ya muziki sanifu (noten).
- Kuhakikisha tumezitunza nyimbo zetu kwa njia ya kurekodi (recording) yaani (Audio) pia kuzipiga kwa ufasaha ili washarika wazijue kuziimba vizuri nyimbo za Tumwabudu Mungu pamoja na Antifoni.
Lengo Kuu La Kikundi
Kuhubiri injili yake Yesu Kristo kwa njia ya uimbaji wa kutumia Tarumbeta na kufanya wanakikundi kuwa pamoja na kwa umoja.
Malengo Ya Kikundi
- Ni kuwa na mfuko kwa ajili ya kikundi ili kusaidia kikundi kisiwe tegemezi kwa vitu vidogo vidogo kwa mfano, ukarabati wa tarumbeta (maintenance) ununuzi wa mafuta kwa ajili ya kulainisha tarumbeta, utoaji wa photocopy ununuzi wa sare za kikundi ili kua na muonekano nadhifu, vifaa vya kufundishia na ununuzi wa vitabu vyenye ubora.
- Kurekodi audio-CD na DVD kwa ajili ya kutunisha mfuko wa kikundi.
- Kuwa na safari za ndani na nje ya Dayosis ili kijifunza na kubadilishana mawazo na vikundi vingine ambavyo vimesonga mbele katika upigaji wa tarumbeta.
Walengwa
- Washarika wa Usharika wa Kijitonyama.
- Washarika nje ya Usharika wa Kijitonyama.
- Washarika wengine nje ya Dayosis.
- Washarika nje ya nchi.
Tarumbeta
Sifa Za Kujiunga na Kwaya
- Awe Mkristo
- Awe Msharika wa Usharika wa Kijitonyama mwenye namba ya ahadi
- Awe mwanajumuiya katika Jumuiya mojawapo hapa usharikani.
- Akubaliane na masharti na kanuni za kikundi
- Atakua chini ya uangalizi wa miezi mitatu kabla ya kuthibitishwa kuwa mwanakikundi kamili.
Ratiba Ya Mazoezi
Mazoezi ya Kikundi ni siku zote kuanzia Jumanne mpaka Jumamosi, saa kumi na nusu jioni hadi saa moja na nusu jioni (10:30 – 1:30 jioni).
Nyimbo / Matoleo Mbalimbali
Toleo | Jina |
Toleo la kwanza | nyimbo za kwaresima |
Toleo la pili | nyimbo za Pasaka(kufufuka) |
Toleo la tatu | nyimbo za kupaa na kushuka kwa Roho Mtakatifu |
Viongozi Wa Kwaya
Cheo | Jina |
Mwenyekiti | Meshack Lema |
M/Mwenyekiti | Mbonea Mokrai |
Katibu | Neema Mushi |
Katibu Msaidizi | Suzan John |
Mtunza Hazina | Happy Kileo |
Mtunza Hazina Msaidizi | Suzan Somi |